MAMBO MATANO YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO YA MAISHA
Maisha ni nini ni hali ya kuitafuta furaha. Binadamu wengi tunapambana ili kuyapata maisha mazuri na yenye furaha wapo walodiriki kuuza viungo vyao ili tu kuileta furaha katika maisha yao
Mambo ya kuzingatia katika maisha
1.Uaminifu na kuwa muwazi. Moja ya vitu vinavyosaidia watu kufanikiwa katika maisha ni uaminifu baina yako na watu walokuzunguka inasaidia kukupa kujuana na watu muhimu kuwa muwazi inasaidia kuaminika kwa haraka vyote hivi vinamchango katika mafanikio ya maisha
2. Kumcha mwenyezi mungu. Swala hili binadamu wengi wanalipuuzia na kusababisha dunia kukumbwa na majanga mengi na kuona kama Mungu amewasahau hapana. Tatizo ni sisi binadamu wa karne hiii tusio mkumbuka hata Mungu muumba wa vyote. Wengi walomtukuza na kumwabudu wamefanikiwa katika maisha yao
3. Kuthubutu kufana jambo pasipo uoga. Maisha haya ya mwanadamu ili kufanikiwa na kuileta furaha katika maisha ni kuthubutu kufanya kitu mfano Biashara,kumpokea kristu,kuacha pombe na mambo mengine yenye mchango hasi na kuthubutu kufanya vitu vyenye mchango chanya
4.Kuacha kabisa tabia ya ubinafsi na kuwa na koyo wa kutoa na kusaidia watu. Mungu hupenda na kubariki watu wanaotoa kwa moyo na kusaidia wenye uhitaji ili umfanya kuzidishiwa zaidi pale anapotoa
5. Epuka imani za kishirikina (uchawi,freemason na miungu mingine) hapa ndipo mungu anapochukia na kukunyima furaha
Comments